mwezi mwandamo

IQNA

IQNA – Kufuatia kuonekana kwa hilali ya mwezi mwandamo jioni ya Jumatano, Alhamisi ilitangazwa rasmi kuwa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani nchini Iran.
Habari ID: 3481956    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/19

IQNA — Wakati baadhi ya nchi za Kiarabu zimetangaza Jumatano kuwa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Waislamu katika mataifa mengine mengi wataanza kufunga Alhamisi.
Habari ID: 3481952    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/18

IQNA-Nchi tatu za Uturuki, Singapore na Oman zimetangaza rasmi kuwa siku ya Alhamisi, tarehe 19 Februari, ndiyo siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3481931    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/13

IQNA – Wakati mamilioni ya Waislamu duniani kote wakisubiri kwa hamu kuwasili kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani na maandalizi yakiendelea, hesabu za kiastronomia zinaonesha kuwa mwisho wa mwezi wa Shaaban 1447 Hijria kiastronomia utasadifiana na Jumatano, Februari 18.
Habari ID: 3481914    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/10

IQNA — Kwa mujibu wa wataalamu wa elimu ya nyota, mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka 2026 kwa hesabu za kiastronomia unatarajiwa kuanza Alhamisi, Februari 19, katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), baada ya kuthibitika kuwa hilali haitoweza kuonekana mapema kuashiria mwanzo wa mwezi huo.
Habari ID: 3481886    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/03

IQNA – Siku ya kwanza ya mwezi wa Shaaban katika kalenda ya Hijria Qamaria ya mwaka 1447 inatarajiwa kuwa Jumatano.
Habari ID: 3481822    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/20

IQNA – Ofisi ya kiongozi mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq, Ayatullah Ali al-Sistani, imetangaza Jumapili, Machi 2, kuwa siku ya kwanza ya Ramadhani katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Habari ID: 3480281    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/01

IQNA - Ofisi ya kiongozi mkuu au Marjaa Taqlid wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq, Ayatullah Ali al-Sistani, imetoa taarifa kuhusu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu. 
Habari ID: 3480244    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/20

Mwezi wa Ramadhani
IQNA - Mahakama kuu ya Saudi Arabia imetoa wito kwa watu wa nchi hiyo kujaribu kufanya Istihlal (kuutafuta mwezi mwandamo ) Jumapili jioni.
Habari ID: 3478480    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/10

TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) amesisitiza kuhusu udharura wa kuungana Waislamu katika kutangaza mwezi mwandamo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3473795    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/09

TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Kimataifa Kimataifa cha Nujumu (IAC) chenye makao yake mjini Abu Dhabi kimetangaza kuwa makadirio yanayoonyesha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 1442 Hijria Qamaria utaanza Aprili 13 2021.
Habari ID: 3473783    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/04

TEHRAN (IQNA) – Baraza la Fiqhi ya Amerika Kaskazini imetangaza kuwa Ijumaa Aprili 24 itakuwa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3472659    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/12

TEHRAN (IQNA)-Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini Oman imetangza kuwa Mei 17 itakuwa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.
Habari ID: 3471500    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/05/07